IQNA

 Wayemeni wajiandaa kwa ajili ya Mfungo wa Ramadhani

17:44 - February 12, 2025
Habari ID: 3480204
IQNA – Kampeni ya kusafisha misikiti kujiandaa kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani imeanzishwa Yemen.

 Kiongozi wa Mamlaka Kuu ya Wakfu, Sheikh Abdulmajeed al-Houthi, aliizindua kampeni ya "Safisha Nyumba Yangu" Jumanne katika Msikiti Mkuu wa mji mkuu Sana'a ili kujiandaa kwa ajili ya Ramadhani.

Kampeni hii inalenga kuhakikisha usafi na matengenezo bora ya misikiti kote Yemen

Sheikh al-Houthi alisisitiza umuhimu wa kutunza misikiti na mchango wao katika kukuza shughuli za kidini na kitamaduni katika jamii.

Aliwataka watu wa makundi yote ya jamii kushiriki katika kampeni hii na kuchangia katika matengenezo ya misikiti.

 

3491832

captcha